• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

Health Services


Mkoa umeendelea kutekeleza Miradi mbali mbali inayolenga kuboresha huduma katika sekta ya Afya. Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na:-


Ujenzi wa zahanati

Mkoa unaendelea kukarabati na ujenzi wa Zahanati.ambapo Ujenzi wa Zahanati 10 umekamilika, maboma 25 yapo hatua ya ukamilishaji na 52 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Ujenzi/Ukarabati wa Vituo vya Afya

 Vituo 9 vimejengwa na kukarabatiwa kwa kuzingatia vipaumbele vya majengo yaliyoelekezwa na Serikali, ambayo ni Jengo la Mtumishi; chumba cha upasuaji; maabara; wodi ya wazazi; chumba cha kuhifadhia miili; na kichomea taka. Vituo hivyo ni kama ifuatavyo:-

1.Ludewa       Mlangali

2.Ludewa       Luilo

3.Ludewa       Manda

4.Ludewa       Makonde

5.Makete        Ipelele

6.Wanging’ombe     Wanging’ombe

7.Wanging’ombe     Palangawanu

8.Makambako         Lyamkena

9.Njombe                MjiIhalula


Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri

Mkoa umeanza ujenzi wa Hospitali za Halmashauri za Wilaya za Wanging’ombe, Njombe, na Mji wa Makambako ambapo ujenzi huo upo katika hatua za mwisho.

 Hospitali za Halmashauri za Ludewa, Njombe Mji na Makete zipo katika mchakato wa kukarabatiwa.


Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa

Mkoa uliandaa andiko la mradi wa ujenzi wa hospitali ambapo Mradi huo uligawanyika katika awamu tano za utekelezaji, ambapo awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD).


Ujenzi wa Nyumba za watumishi katika Vituo vya Afya na Zahanati.

Mkoa unaendelea na ujenzi wa Nyumba 22 za watumishi ambazo ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Huduma za Uzazi na Mtoto

Mkoa umefanikiwa kuviwezesha vituo 258 kutoa huduma ya uzazi na mtoto kati ya vituo 280, na kuongeza vituo vinavyotoa huduma za upasuaji wa dharura kutoka Vituo 8 mwaka 2013 hadi Vituo 17 mwaka 2018.

Kutokana na ongezeko hilo, vifo vya akina mama wajawazito vimepungua kutoka akina mama 250 kwa kila vizazi hai 100,000 (250/100,000) mwaka 2005 hadi kufikia vifo 101.81kwa kila vizazi hai 100,000 (101.81/100,000) mwaka 2018. Aidha, vifo vya watoto watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka   watoto 51 kwa kila vizazi hai 1,000 (51/1,000) mwaka 2005 hadi kufikia vifo 5 kwa watoto 1,000 (5/1,000) mwaka 2018.

Mapambano Dhidi ya UKIMWI

Mkoa umefanikiwa kuongeza Vituo vinavyotoa huduma za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) toka vituo 13 mwaka 2012 hadi kufikia vituo 258 mwaka 2018. Sambamaba na kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupungua kutoka asilimia 9.5 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 2 mwaka 2018.


Aidha, Mkoa umeongeza Vituo vinavyotoa huduma ya tiba na matunzo kutoka Vituo 21 Mwaka 2010 hadi vituo 101 Machi, 2019  Hivyo kufanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 14.8 (THMIS 2011/12) hadi asilimia 11.6 (THIS 2016/2017), japo bado Mkoa unaongoza kwa maambukizi ya VVU na UKIMWI Kitaifa.

Usafi wa Mazingira

Mkoa unatekeleza mikakati mbalimbali ya Kampeni ya usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na agizo lako Mhe. Rais la wananchi kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi ya kila Mwisho wa mwezi.

Kampeni ya usafi wa mazingira imeuwezesha Mkoa kutopata mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao uliathiri Mikoa mingi nchini mwaka 2015, 2016 na 2017 na 2018.

Aidha, katika Kampeni ya Kitaifa ya usafi wa Mazingira, Mkoa umekuwa ukipata ushindi wa nafasi ya kwanza hadi ya nne katika Halmashauri za Wilaya na Miji Tanzania Bara mfululizo kuanzia mwaka 2014 hadi 2018 kwa kutoa vijiji bora vya usafi wa Mazingira katika Halmashauri za Wilaya ya Njombe na Makete. Kutokana na ushindi huo, Halmashauri zilipata zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyeti vya ushindi, vikombe, matrekta kwa ajili ya kuzoa taka Mjini, magari na pikipiki.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 MKOA WA NJOMBE December 14, 2022
  • View All

Latest News

  • ZIARA YA MKUU WA MKOA NJOMBE YA ZAA MATUNDA

    January 19, 2023
  • WAZIRI WA KILIMO AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA NJOMBE

    January 18, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA

    November 27, 2022
  • ZIARA

    November 26, 2022
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Njombe Nearby Ruhuji River

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 0262782912/13

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.