Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Njombe, Ndugu. Lewis Mnyambwa leo tarehe 9 Januari, 2025 ametembelea mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika vituo vya Mlangali na Ludewa vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani humo.
Ndugu Mnyambwa amewaasa washiriki hao kufanya kazi yao kwa weledi, uadilifu na kutumia lugha nzuri kwa waandikishwaji watakaofika kituoni.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari utakaofanyika katika mikoa ya Songwe, Njombe, Rukwa kwa siku saba kuanzia Januari 12, 2025 hadi Januari 18, 2025, ambapo vituo vitakuwa vikifunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.