• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

RC MTAKA AFANYA MAZUNGUMZO YA KIUCHUMI NA VIONGOZI WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI TANZANIA

Posted on: January 13th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amekutana na viongozi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC-TZ) waliofika mkoani humo kwa ziara ya mafunzo ya washiriki wa Kozi ya Kumi na Nne. Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mitaala ya mafunzo ya ulinzi na usalama wa taifa.

‎

‎Akizungumza katika kikao hicho, Mtaka amesema Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa inayochangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Tanzania kutokana na uwepo wa shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazofanywa na wakazi wake. Ameeleza kuwa mkoa huo una rasilimali muhimu ikiwemo madini yenye thamani kubwa, hususan miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma ya Liganga.

‎

‎Mtaka amefafanua kuwa Serikali tayari imeshalipa fidia kwa wakazi wa maeneo yanayotekelezwa miradi ya Mchuchuma na Liganga, akibainisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni miongoni mwa alama kubwa zitakazokumbukwa katika uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

‎

‎Ameongeza kuwa miradi hiyo imeingizwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025–2050 na imepewa kipaumbele cha juu miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo Serikali imeelekeza nguvu na rasilimali zake ili kuhakikisha inatekelezwa kikamilifu.

‎

‎Kwa upande wake, Kiongozi wa msafara wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Brigedia Jenerali PN Songea, amesema ziara hiyo inalenga kuwapatia washiriki uelewa wa vitendo kuhusu utekelezaji wa sera, mipango na miradi ya Serikali, pamoja na majukumu ya taasisi mbalimbali za umma na binafsi katika kulinda usalama na kuharakisha maendeleo ya taifa.

‎

‎Brigedia Jenerali Songea ameeleza kuwa Kozi ya Kumi na Nne inahusisha washiriki 72 kutoka mataifa 17, wakiwemo Watanzania pamoja na washiriki kutoka nchi rafiki. Amebainisha kuwa hali hiyo inaifanya kozi hiyo kuwa jukwaa la kimataifa la kujadili masuala ya ulinzi, diplomasia, usalama na maendeleo.

‎

‎Katika ziara hiyo mkoani Njombe, washiriki wamepata fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Serikali inavyotekeleza sera zake, pamoja na changamoto na fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali ya nchi.

‎

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MKOA WA NJOMBE UMEPANDA JUMLA YA MITI 400 HALMASHAURI YA MAKAMBAKO

    January 19, 2026
  • JUMUIYA YA WADAU WA PARACHICHI WAFANYA MKUTANO WAO WA MWAKA

    January 17, 2026
  • RC MTAKA AFANYA MAZUNGUMZO YA KIUCHUMI NA VIONGOZI WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI TANZANIA

    January 13, 2026
  • WADIWANI WAPEWA MAFUNZO YA UONGOZI TAYARI KWA KUANZA MAJUKUMU YAO

    January 16, 2026
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.