• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

WAZIRI BALOZI DKT. PINDI CHANA AWAONGOZA WATANZANIA KUMUENZI MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE KUPITIA MBIO ZA HIYARI (MWL.NYERERE MARATHON)

Posted on: October 1st, 2022

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi leo Oktoba 1, 2022 wilayani Butiama mkoani Mara amezindua rasmi mbio za hiyari za Mwl. Nyerere Marathon ikiwa ni sehemu ya kuenzi, kutangaza na kuhifadhi historia adhimu na adimu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Mbio hizo zimewahusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo washiriki wa mbio hizo wamekimbia kupitia njia alizotumia Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere kwenda Shule na shughuli zake za kila siku akiwa Butiama.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa chimbuko la mbio hizo ni Mpango wa Miaka 10 ya kumuenzi na kutangaza urithi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani na nje ya Tanzania

“ Mwalimu Nyerere Marathon itakua endelevu na itafanyika kila mwaka hapa Butiama kupitia njia ambazo Baba wa Taifa alizitumia kwenda shule ya Msingi Mwisenge ili kutangaza na kuhifadhi historia adhimu ya Baba wa Taifa” Amesisitiza Balozi Dkt. Pindi Chana.

Ameongeza kuwa uwepo wa mbio hizo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ibara ya 71 (g) inayoelekeza kuhifadhi maeneo muhimu ya kihistoria hapa nchini yakiwemo ya Mwalimu Nyerere ambayo ni urithi wa utamaduni wa Taifa, vivutio vya Utalii pamoja na Utafiti.

Aidha, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameeleza kuwa mbali na kutangaza urithi na historia, mbio hizo za hiyari ni zao jipya la utalii kupitia michezo vile vile zimelenga kukusanya michango ya fedha za hiyari kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya makumbusho na vituo vya malikale vya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambavyo vinaratibiwa na Makumbusho ya Taifa la Tanzania.

Wakati wa mbio hizo za Mwl. Nyerere Marathon 2022, viongozi, wananchi na wadau mbalimbali wamejitokeza kuungana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana na Naibu wake Mhe. Mary Masanja kwenye mbio hizo kumuenzi muasisi wa Taifa la Tanzania kwa vitendo ambapo wakimbiaji wamekimbia Kilomita 22, 13 na Kilomita 4 kuashiria tarehe, mwezi na mwaka aliozaliwa Baba wa Taifa Mwalimu  Julius Kambarage Nyerere.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 MKOA WA NJOMBE December 14, 2022
  • View All

Latest News

  • ZIARA YA MKUU WA MKOA NJOMBE YA ZAA MATUNDA

    January 19, 2023
  • WAZIRI WA KILIMO AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA NJOMBE

    January 18, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA

    November 27, 2022
  • ZIARA

    November 26, 2022
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Njombe Nearby Ruhuji River

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 0262782912/13

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.