• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

ZIARA YA MKUU WA MKOA NJOMBE YA ZAA MATUNDA

Posted on: January 19th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthon Mtaka amefanya ziara ya kikazi leo katika   halmashauri ya Mji Njombe Kata ya Ramadhani mtaa wa Mgodechi,Kufuatia kukamatwa kwa shehena ya mifuko ya mbolea inayodaiwa kutumika kufanya uchakachuaji na udanganyifu leo hii, kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Njombe ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Antony Mtaka wamefika kwa wakulima walionunua mbolea siku chache zilizopita na waliokiri kununua mbolea iliyofanyiwa udanganyifu kutoka kwa mfanyabiashara jina lake limehifadhiwa anayeshukiwa kukutwa na shehena hiyo ya mifuko inayokadiliwa kuwa zaidi ya 10,000.

Zoezi hilo limefanyika leo Januari 19, 2023 katika mtaa wa Mgodechi pembezoni kidogo ya mji wa Njombe kukutana na wakulima ambako pia kunapatikana moja ya duka la mfanyabiashara anayedawa kuuza mbolea feki,walisema kuwa mbolea hiyo ilikua na utofauti na mbolea nyingine ambazo wamewahi kutumia.

Ibrahimu kilunde mkulima wa viazi alisema mbolea hiyo ilikua tofauti na mbolea ambazo wamezoea kutumia kwenye msimu uliopita wa kilimo.

"Tulinunua ya kupandia na kukuzia madhara yake nimeyaona,mazao yananyauka kingine hata ardhi yenyewe itapata madhara kwa sababu tumetumia mara kwa mara,kuna mabadiliko ya rangi ina rangi zaidi ya tatu na ya zamani ilikua a rangi moja kama nyeupe ni nyeupe kama nyeusi inakua nyeusi"alisema

Zawadi Mgaya alisema kuwa mbolea hiyo inaujazo mdogo kuliko mbolea nyingine."Mimi nilinunu mifuko minne hadi sasa hivi ninayo nyumbani,ujazo ni mdogo sana ukilinganisha na mifuko mingine ambayo tuliwahi kununua sehemu nyingine"alisema Mgaya.

Kwa upande Adelina Stewele alisema alivyofika dukani aliomba kuuziwa mbolea aina ya DAP mifuko miwili lakini alivyofika nyumbani alikuta iko tofauti.

"Nilivyofika nyumbani wakati nafungua nakuta sio DAP na mbolea yenyewe nimetembea nayo hii hapa"alisema.

Aliongeza kuwa"Hata ujazo haijajaa,mfuko kawaida unashinwa mshono mmoja sasa huu ulikua umeshonwa mara mbili ukiwa umepinda pinda"alisema.

Geresius Ng'ande alisema alinunua DAP mifuko miwili"Wakati naweka kwenye shamba nakuta yani hayeyuki nikauuliza hii safari hii ni mbolea aina gani mbona ni vumbi nikafungua mwengine nao nikakuta ni vumbi kwa hiyo nikashindwa nikakuta habari kwamba vijana wamebaini mbolea feki"alisema Ng'ande.

Exaud Mgina alisema alipokwenda kununua mbolea hiyo aligundua utofauti na alipokwenda kuuliza dukani aliambiwa asubiri atabadilishiwa.

Kufuatia mkutano huo wakulima waliokumbwa na kadhia ya kuuziwa mbolea bandia wakatakiwa kurudi majumbani kwao na kujitokeza na mifuko waliyonunua kwa mfanyabiashara huyo.

Hata hivyo kulifanyika upimaji wa mbolea hizo na afisa udhibiti ubora wa mbolea TFRA nyanda za juu kusini Chimile Mfugale alibaini majina ya mbolea kwenye vifungashio ni tofauti na mbolea iliyopo ndani ya mfuko huku mbolea nyingine ikiwa na mchanganyiko usioeleweka.

Aidha mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka aliwataka wananchi wote ambao wameuziwa mbolea hizo kujiandikisha majina kwa ajili ya kufanyiwa fidia.

"Jana kwenye nyumba ya huyu mfanyabiashara tulikamata mifuko elfu 10,532 ambayo ilikua ni mifuko imetoka kiwandani ni mitupu lakini yameandikwa majina ya hizi mbolea maana take alikua anafanya kazi ya kupriiti hii mifuko anakuja anachakachua anaandika minjingu kumbe DAP anaandika DAP kumbe minjingu anakuja anauza kernye maduka yake kama zoezi lile lingefanikiwa maana angefanya uchakachuaji wa mbolea kama alivyokua anauza hapa dukani kwa mifuko ile angefanikiwa angepata shilingi milioni 737,240,000"alisema.

Hata hivyo mkuu wa mkoa alisisitiza kutafutwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola mfanyabiashara huyo.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 MKOA WA NJOMBE December 14, 2022
  • View All

Latest News

  • ZIARA YA MKUU WA MKOA NJOMBE YA ZAA MATUNDA

    January 19, 2023
  • WAZIRI WA KILIMO AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA NJOMBE

    January 18, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA

    November 27, 2022
  • ZIARA

    November 26, 2022
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Njombe Nearby Ruhuji River

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 0262782912/13

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.